Kiongozi wa upinzani Zambia amesema anaendelea vema kuzuizini
Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema, anayeendelea kuzuiliwa jijini Lusaka kwa makosa ya uhaini, wiki hii amesema anaendelea vema kuzuizini.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Hichilema amewaambia wafuasi wake kuwa yeye pamoja na wenzake wanaozuiliwa wapo katika hali nzuri licha ya jitihada zinazoendelea kuwafanya wakate tamaa.
Aidha, amesema anachotaka ni ukweli ubainike Mahakamani na kuongeza kuwa wanachofanya ni kupigania demokrasia nchini mwao.
Mwanasiasa huyo alikamatwa na ku kufunguliwa mashtaka miezi miwili iliyopita, baada ya kutuhumiwa kuzuia masafara wa rais Edgar Lungu madai ambayo ameyakanusha.
Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka uliopita, ambao Lungu alitangazwa mshindi, Hichilema alidai kuibiwa kura na hivyo kukataa kumtambua kama kiongozi wa nchi hiyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |