• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (24 Juni-30 Juni)

    (GMT+08:00) 2017-06-30 18:57:42

    Umoja wa Ulaya waongeza muda wa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Russia kwa miezi sita

    Baraza la Umoja wa Ulaya limetangaza kuongeza muda wa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Russia hadi tarehe 31 mwezi Januari mwakani kutokana na hali mbaya ya utekelezaji wa mkataba wa Minsk.

    Vikwazo hivyo ni pamoja na kuyazuia mashirika matatu ya nishati, mashirika matatu ya ulinzi, mashirika matano ya kifedha ya Russia kuingia soko la mitaji la Umoja wa Ulaya, kupiga marufuku ya biashara ya silaha kati ya Umoja wa Ulaya na Russia, kuizuia Russia kupata teknolojia na huduma kwenye sekta ya uchimbaji na uzalishaji wa mafuta, na kuzuia kuiuzia Russia bidhaa za kiraia ambazo pia zinaweza kutumiwa kwa malengo ya kijeshi.

    Umoja wa Ulaya umeiwekea Russia vikwazo vya kiuchumi tangu mwezi Julai mwaka 2014 kutokana na madai kuwa Russia inahusika na ukosefu wa usalama katika eneo la mashariki mwa Ukraine.

    Wakati huo huo Waziri mkuu wa Russia Bw. Dmitry Medvedev amesema serikali ya Russia inapanga kuongezea muda hatua za kupambana na vikwazo ilivyowekewa na Umoja wa Ulaya hadi kufikia mwishoni mwa mwaka kesho, ili kujibu hatua ya Umoja wa Ulaya kuongeza muda wa vikwazo dhidi ya Russia.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako