Trump na Putin kukutana wiki ijayo G20
Ikulu ya Marekani imethibitisha kuwa Rais Donald Trump atakutana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wiki ijayo, ikiwa ni maandalizi ya mkutano wa nchi 20 zilizoendelea zaidi kiuchumi duniani (G20).
Itakuwa mkutano wa kwanza wa ana kwa ana baina ya viongozi hawa wawili.
Mshauri wa masuala ya ulinzi wa Marekani H.R. MacMaster amesema bado hakuna mada maalumu iliyopendekezwa.
Mapema msemaji wa ikulu ya Kremlin alithibitisha uwepo wa mkutano huo
Aidha Wizara ya mambo ya nje ya China imetoa taarifa kuwa rais Xi Jinping wa China atafanya ziara nchini Russia na Ujerumani, na kuhudhuria mkutano wa kilele wa 12 wa kundi la nchi 20 kuanzia tarehe 3 hadi tarehe 8 Julai.
Msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Li Huilai amesema, nchini Russia rais Xi Jinping atakutana na rais Vladmir Putin na kuhakikisha mwelekeo na lengo la maendeleo ya uhusiano kati ya China na Russia, kuzidisha uaminifu wa kisiasa na kimkakati, kusukuma mbele ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |