• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (10 Julai-14 Julai)

    (GMT+08:00) 2017-07-14 19:26:47
    Rais wa Sudan Kusini awafukuza kazi majaji wa ngazi ya juu wakati mgomo ukiendelea

    Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini wiki hii amewafukuza kazi majaji 12 wa ngazi ya juu wakati mgomo ukiendelea uliofanya shughuli za mahakama katika nchi hiyo kusimama.

    May Mosi, majaji walianza mgomo wakidai kufutwa kazi kwa Jaji Mkuu Chan Reec Madut, mshirika mkuu wa rais Kiir ambaye wanamtuhumu kwa utendaji mbovu na kupunguza nguvu ya mahakama.

    Pia majaji hao wanalalamikia kucheleweshwa kwa mishahara na mazingira mabovu ya kazi.

    Katikati ya mwaka jana, walimu na wahudumu wa afya nchini Sudan Kusini waligoma kwa madai ya nyongeza ya mishahara na mazingira duni ya kazi, lakini baadaye walirudi kazini.

    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako