Uingereza yaulaumu Umoja wa Ulaya kwa kudai malipo makubwa ya Brexit
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Bw. Boris Johnson jana kwenye baraza la chini la bunge la Uingereza amesema, Umoja wa Ulaya unadai malipo makubwa kwa Uingereza kujitoa umoja huo, ambayo Uingereza haikubali.
Hii ni mara ya kwanza kwa Uingereza kuonesha msimamo imara kwenye suala la malipo ya kujitoa Umoja wa Ulaya tangu mazungumzo ya Brexit yaanze.
Bw. Johnson pia amesema, serikali ya Uingereza bado haijaandaa mpango mbadala kwa ajili ya uwezekano wa kushindwa kufikia makubaliano yoyote na Umoja wa Ulaya, hali inayomaanisha kuwa hata kama Uingereza haitaweza kufikia makubaliano ya kibiashara na Umoja wa Ulaya, pia itajitoa kwenye soko la pamoja la Ulaya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |