Chama tawala Rwanda kuanza kampeni za urais
Chama tawala cha Rwanda Patriotic Front RPF kimetangaza kuanza kampeni za urais ijumaa katika mkoa wa Kusini.
Mwezi uliopita Chama cha RPF kilimchagua rais wa sasa Paul Kagame wa Rwanda kuwa mgombea urais wa chama hicho, atakayeshindana na Frank Habineza wa chama cha kijani, na mgombea huru Philipe Mpayimana.
Katibu mkuu wa chama cha RPF Bw Francois Ngarambe amesema RPF itafanya kampeni nchini kote na kuwafahamisha wananchi wa Rwanda mipango yake katika miaka saba ijayo.
Kampeni za uchaguzi zitaanza rasmi tarehe 3 mwezi ujao wilayani Ruhango, mkoa wa Kusini.
Nako nchini Kenya sasa imesalia chini ya mwezi mmoja tu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu Agosti nane.
Wanasiasa wameendelea na kampeni zao nchini humo huku kinyang'yaniro kikali kwenye kiti cha urais kikiwa ni kati ya Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee na aliyekuwa waziri Mkuu Raila Odoinga anayeongoza muungano wa NASA.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |