Korea Kaskazini kuiachilia meli ya uvuvi ya Korea Kusini .
Korea Kaskazini inasema kuwa itaiachilia meli ya uvuvi ya Korea Kusini ilioikamata siku sita zilizopita kwa kuingia katika himaya yake kinyume cha sharia.
Chombo cha habari cha KCNA kimesema meli hiyo na wafanyikazi wake itaachiliwa katika mpaka wa kijeshi katika bahari ya mashariki.
Uamuzi huo ulitolewa baada ya wafanyikazi hao kuomba msamaha kwa kufanya makosa hayo.
Hatua hiyo inajiri wakati ambapo kuna wasiwasi katika eneo hilo huku pande zote mbili zikifanya mizururu ya mazoiezi ya kijeshi.
Korea Kaskazini imesema kuachiliwa kwa meli hiyo ya uvuvi, baadaye siku ya Ijumaa inafuatia hatua ya kukiri makosa kwa wale waliokuwa wakiabiri chombo hicho ambao walitaka serikali ya Korea Kaskazini kuwavumilia.
Uchunguzi, kulingana na Korea Kaskazini, ulithibitisha kuwa wavuvi hao waliingia maji ya taifa lake siku ya Jumamosi.
Wakati huo huo Wizara ya fedha ya Marekani imetangaza vikwazo vipya dhidi ya watu binafsi saba na mashirika matatu ya Korea Kaskazini kutokana na kuhusika na ilichodai kuwa ni ukiukaji wa haki za binadamu. Watu binafsi waliowekewa vikwazo hivyo ni pamoja na maofisa wa usalama wa jeshi la Korea Kaskazini, waziri wa leba Jong Yong Su, konsela mkuu wa nchi hiyo mjini Shenyang, na mwanadiplomasia mwingine katika ubalozi wake nchini Vietnam.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |