Ethiopia yatuma walinzi 200 wa amani Sudan Kusini
Ethiopia imetuma askari 200 wa kulinda amani Sudan Kusini, ili kusaidia kuimarisha amani nchini humo hayo ni kwa mujibu wa Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia Bw. Meles Alem .
Bw. Alen amesema askari hao wametumwa kutokana na azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu kusaidia kuimarisha amani ya Sudan Kusini.
Mwezi Desemba mwaka jana baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio nambari 2327 kuhusu kuongeza nguvu ya Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, ambalo limeamua kurefusha muda wa tume hiyo hadi mwishoni mwa mwaka huu, na kutoa agizo kali kwa tume hiyo kuwalinda raia wa Sudan Kusini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |