• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (21 Oktoba-27 Oktoba)

    (GMT+08:00) 2017-10-27 18:17:15

    Uchaguzi wa urais Kenya wafanyika huku kukiwa na maandamano ya upinzani

    Kenya imeandaa uchaguzi mpya wa urais alhamis ambao umesusiwa na upinzani.

    Wafuasi wa upinzani wamekuwa wakifanya maandamano kupinga uchaguzi huo huku polisi wakiimarisha doria katika maeneo mengi nchini humo.

    Rais Uhuru Kenyatta amewataka wakenya kudumisha amani wakati na baada ya zoezi hilo.

    Maduka mengi yamesalia kufungwa, na barabara nyingi hazina msongamano wa magari.

    Vituo vya kupigia kura nchini Kenya vilifunguliwa alfajiri saa kumi na mbili Alhamisi.

    Lakini sio kwenye vituo vyote ambako wapiga kura walijitokeza hasa kwenye maeneo kwenye wafuasi wengi wa muungano NASA.

    Muungano huo tayari ulikuwa umetangaza kwamba hautashiriki kwenye zoezi hilo la marudio ya kura ya urais wakilalamikia kutokuwepo na mageuzi kwenye tume huru ya uchaguzi IEBC.

    Jumatano mahakama nchini Kenya ilitoa uamuzi kwamba uchaguzi unafaa kuendelea hata kama mgombea mmoja amejiondoa.

    Leo akipiga kura katika eneo bunge la Gatundu kusini, Kenyatta aliwaomba wakenya kudumisha amani wakati na baada ya uchaguzi.

    Wawekezaji wenyeji wa Kenya wamesema, nchi hiyo imepoteza dola bilioni 7 za kimarekani katika miezi minne iliyopita kutokana na hali ya sintofahamu ya kisiasa kuhusiana na uchaguzi.

    Shirikisho la Sekta ya Binafsi la Kenya (KEPSA) limesema shughuli za kiuchumi kati ya mwezi Julai na Oktoba nchini humo zimeshuka kutokana na wasiwasi kuhusu uchaguzi.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako