Watu 14 wapoteza maisha katika shambulio la bomu Mogadishu
Watu 14 wamekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa siku ya Alhamisi wakati gari lilipolipuka nje ya hoteli moja maarufu ijini Mogadishu, Somalia.
Kundi la Al-Qaeda lenye uhisiano na wapiganaji wa Al-Shabab nchini Somalia limekiri kuhusika kwenye shambulio la mbele ya hoteli ua Weheliya katikati mwa mji wa Mogadishu, kundi hilo likidai lililenga mkutano wa viongozi wa Serikali.
Msemaji wa Serikali amesema watu 14 walipoteza maisha kwenye eneo la tukio na kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka wakati huu vikosi vya uokoaji vikiendelea kutafuta miili zaidi.
Watu walioshuhudiwa tukio hilo wanasema ulitokea kwenye mtaa wa Makkah al-Mukarama moja ya mitaa ambayo inashughuli nyingi kuunganisha na eneo la kati la mji wa Mogadishu.
Mji wa Mogadishu umekuwa ukilengwa na mashambulizi ya mara kwa mara yanayotekelezwa na kundi la Al-Shabab linalopigana kuiangusha Serkali ya Somalia inayotambuliwa kimataifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |