• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 17-March 23)

    (GMT+08:00) 2018-03-23 17:44:45

    Sarkozy ashtakiwa rasmi kwa rushwa

    Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amefunguliwa rasmi mashtaka ya rushwa na ufadhili wa kinyume cha sheria wa kampeni kuhusiana na tuhuma kuwa kiongozi wa zamani wa Libya marehemu Kanali Muammar Gaddafi alisaidia kufadhili kampeni zake za urais mwaka 2007.

    Baada ya miaka mitano ya uchunguzi na siku mbili za kuhojiwa na polisi akiwa chini ya ulinzi, majaji wanaochunguza kashfa hii kubwa ya kisiasa kuwahi kushuhudiwa nchini Ufaransa waliamua kuwa wanao ushahidi wa kutosha kumshtaki Sarkozy mwenye umri wa miaka 63.

    Sarkozy ambaye alihudumu kwa muhula mmoja tu kati ya mwaka 2007 na 2012, alishtakiwa kwa rushwa, ufadhili haramu wa kampeni na kutumia fedha mali ya uma ya Libya, amesema mtoa taarifa mmoja kwenye uchunguzi huo.

    Taarifa zinasema kuwa sarkozy aliruhusiwa kurudi nyumbani jana jioni baada ya kumaliza kuhojiwa.

    Hata hivyo Sarkozy mwenyewe ameendelea kukanusha mashtaka yanayomkabili na ambayo yamekuwa yakimuandama tangu aondoke madarakani mwaka 2012.

    Kiongozi huyu sasa atakuwa na muda wa miezi 6 kukata rufaa dhidi ya mashtaka yanayomkabili, hatua ambayo anatarajiwa kuichukua na majaji watalazimika kufanya uamuzi zaidi kuamua ikiwa wanaushahidi wa kutosha kuendelea na kesi.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako