China yaahidi kutoa zaidi ya dola bilioni 60 kwa Afrika
Rais Xi Jinping, wa China ameahidi Jumatatu wiki hii kwamba China itatoa zaidi ya dola bilioni 60 kwa maendeleo ya kiuchumi ya nchi za Afrika,
Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kilele wa baraza la ushirikiano kati a China na Afrika FOCAC lililofanyika katika mji mkuu Beijing.
Xi Jinping ameongeza kwamba fedha zitakazotolewa zitajumuisha dola bilioni tano ya mikopo isiyokuwa na riba na dola bilioni 35 ya mikopo ilio na mashrti nafuu itakayotolewa kwa Afrika.
Katika hotuba yake ya ufunguzi kwenye mkutano huo, Xi pia alitangaza msaada wa kupambana na ukame barani Afrika na kutangaza kuwa china itatoa dola milioni 156 ya kushughulikia msaada wa vyakula vya dharura katika maeneo yatakayoathirika.
Rais huyo wa China amesema nchi yake pia itaimarisha ushirikiano wake barani Afrika katika vita vyake dhidi ya makundi yalio na itikadi kali na imesema haitoingilia michakato ya kiasiasa ya serikali za bara hilo.
Aidha rais Jinping amebaini kwamba makampuni ya China yatatakiwa kuwekeza "angalau dola bilioni 10" barani Afrika kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |