Kuongezwa kwa kodi kwasababisha uhaba wa mafuta Kenya
Tume ya kudhibiti nishati nchini Kenya imefuta leseni ya muungano wa wafanyabiashara wanoagiza mafuta KIPEDA ikiwalaumui kwa kuvuruga uchumi.
Wiki hii kumekuwa na uhaba wa mafuta baada ya wasambazaji kugoma wakilalamikia kuongezwa kwa ushuru wa asilimia 16.
Zimeshuhudiwa foleni ndefu kwenye mji mkuu Nairobi na viunga vyake wakati wenye magari wanasubiri kuongeza magari yao mafuta.
Wauzaji na wasafirishaji mafuta wamekuwa wakisusia katika jitihada za kuishinikiza serikali ifute kodi mpya. Uhaba wa mafuta umeshuhudiwa sehemu tofauti za nchi.
Hii inajiri huku shinikizo zinazidi kumuandana Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta za kumtaka aweke sahihi mswada wa uchumi mwaka 2018 wenye mabadiliko ya kufuta kodi mpya iliyowekwa kwa bidhaa za mafuta.
Kodi hiyo ya asilimia 16 ilitangazwa na wizara ya fedha, licha ya mswada uliopitishwa na bunge ambao ulitupilia mbali kodi hiyo kwa miaka miwili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |