Viongozi wa Korea Kusini na Korea Kaskazini kukutana mjini Pyongyang baadaye mwezi huu
Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wanatarajiwa kukutana tarehe 18 hadi 20 mwezi huu mjini Pyongyang.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Korea Kusini imesema, wajumbe kutoka Korea Kusini na Korea Kaskazini wamejadiliana na kufikia makubaliano kuhusu mkutano wa viongozi hao.
Mkurugenzi wa idara ya usalama ya ikulu ya Korea Kusini Bw. Chung Eui-yong amesema, viongozi hao watatathmini matokeo ya utekelezaji wa azimio la Panmunjom na kujadili mwelekeo wa utekelezaji huo.
Pia watajadili masuala ya amani na ustawi wa kudumu wa peninsula ya Korea, hasa suala la mpango wa utekelezaji wa kuondoa silaha za nyuklia katika peninsula hiyo.
Pande hizo mbili zitafanya mkutano wa ngazi ya juu mwanzoni mwa wiki ijayo kujadili maandalizi ya mkutano huo muhimu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |