Maambukizi mapya ya Ebola yasababisha vifo vya watu 100 nchini DRC
Takwimu mpya zilizotolewa na Wizara ya Afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC zimeonesha kuwa, hadi sasa watu 100 wanashukiwa kufariki kutokana na ugonjwa wa Ebola mkoani Kivu Kaskazini, mashariki mwa nchi hiyo, huku vifo 69 kati ya hivyo vikithibitishwa kutokana na maambukizi hayo.
Takwimu hizo zimeonesha kuwa, wagonjwa 150 wanashukiwa kuwa na maambukizi ya virusi hivyo na 119 kati yao wamethibitishwa kuambukizwa na virusi hivyo.
Maambukizi hayo yametokea katika sehemu yenye vurugu ya nchi hiyo, ambayo kazi ya kinga na udhibiti inakabiliwa na ugumu, hivyo kuifanya timu inayoshughulika na kinga na udhibiti wa maambukizi hayo kusitisha baadhi ya huduma kutokana na athari zinazotokana na mapigano.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |