Vifo kutokana ajali ya kuzama kwa kivuko nchini Tanzania vyafikia 218
Vifo kutokana na ajali ya kuzama kwa kivuko kwenye ziwa Victoria nchini Tanzania vimeongezeka na kufikia 218 na kuna uwezekano idadi hiyo ikaongezeka.
Kwa mujibu wa waziri wa Kazi, Usafirishaji na mawasiliano, Isack Kamwelwe miili Zaidi inaweza kupatikana kwa kuwa shughuli za uokoaji na uopoaji zinaendelea.
Aidha waziri huyo amesema tayari shughuli za ndugu kutambua miili ya wapendwa wao zinaendelea, na akiwaambia waandishi wa habari kuwa meli kubwa iliyobeba mitambo kwa ajili ya kuvuta kivuko hicho kilichozama inatarajiwa kuwasili na kuanza kufanya kazi.
Wakati huo huo kivuko hicho kimenyanyuliwa wiki hii na kuwekwa sawa ikiwa ni siku tano tangu kazi hiyo ilipoanza.
Kivuko hicho kimenyanyuliwa baada ya jitihada za siku tano, tangu Jumapili iliyopita ambako wataalamu wa uokoaji kutoka vyombo vya ulinzi na usalama wakiongozwa na maofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakishirikiana na makundi mbalimbali ya uokoaji wa ndani na nje ya Mkoa wa Mwanza.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |