Joseph Kabila aonya nchi za kigeni kungilia katika masuala ya DRC
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila Kabange ameonya nchi za kigeni kwa kile alichokitaja "kuingiliwa katika masuala ya nchi yake, na kuomba kwa mara nyingine Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (Monusco) kuondoka nchini humo.
Kauli hiyo aliitoa katika mkutano Mkuu wa 73 wa Umoja w Mataifa huko New York nchini Marekani. Mkutano ambao ulianza tangu Jumanne wiki hii.
Joseph Kabila ameelezea ahadi yake kwa maadili yaliyotetewa na Umoja wa Mataifa, huku akishtumu baadhi ya nchi za kigeni kuingilia katika masuala ya ndani ya nchi yake.
Rais Kabila amesema DRc imekua sasa na amani na utulivu , huku akiomba akisisitiza Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (Monusco) kuanza kuondoa askari wake nchi humo.
Kauli hii inakuja wakati serikali ya DRC, hasa majeshi yake yameendelea kukosolewa kushindwa kudhibiti usalama katika maeneo mengi ya nchi, hasa katikamikoa ya Kivy Kaskazini, Kivu Kusini, na Tanganyika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |