Wachimba migodi 16 watekwa Nigeria
Wachimba migodi kumi na sita wametekwa nyara na kundi la wahalifu kaskazini mwa Nigeria, katika eneo linalojulikana kwa visa hivyo ambapo watekaji nyara wamekuwa wakiomba fidia kwa familia za mateka , polisi na wakuu wa eneo hilo wamesema.
Watu hao walitekwa Jumanne usiku walipo kuwa njiani wakirudi kutoka mgodini katika eneo la Birnin Gwari katika Jimbo la Kaduna, msemaji wa polisi Yakubu Sabo amesema.
Amesema wachimba migodi 16 walikuwa wakisafiri kwa lori wakati walipovamiwa karibu na kijiji cha Bogoma na kundi la wahalifu ambao waliwapeleka mahali pasipojulikana.
Kwa mujibu wa Abdullahi Bature, msemaji wa kiongozi wa jadi wa Birnin Gwari, Zubairu Mai-Gwari, kisa hicho cha utekaji nyara kilitokea wakati gari waliokuwemo ilikuwa imeegesh akando ya barabara baada ya kupatwa na tatizo.
Bature amesema, kuwa watekaji nyara hao waliwasiliana na familia za mateka wakiomba pesa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |