Wahamiaji 60 wafa maji Guinea Bissau
Takribani wahamiaji 60 wanahofiwa kufa maji baada ya boti waliokua wakisafiria kupigwa na dhroruba na kupinduka huko Guinea Bissau.
Vikosi vya majini vimeshindwa kuwasaidia baada ya boti hiyo kuzama siku ya jumatatu kufuatiwa na ukosefu wa vifaa vya kuokolea.
Mkuu wa mamlaka ya bandari wa taifa amesema , baadhi ya mabaki ya boti hiyo yamepatikana lakini hakuna miili iliyoweza kutambulika.
Haijajulikana ni wapi boti hiyo ilipokua inaelekea lakini ilikua ikikatisha kisiwa cha Kanari huko Uhispania ambapo ni kilomita 1,120 kutoka Guinea Bissau.
Ajali nyingi za majini za wahamiaji zinasababishwa na kujaa watu na mizigo na wengi wa wahamiaji ni vijana ambao wanashindwa kupata kazi na kuamua kwenda nchi za nje kutafuta maisha bora.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |