Waliofariki kutona na Tsunami Indonesia wafikia 1,400
Idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia tetemeko la ardhi na Tsunami katika Kisiwa cha Celebes nchini Indonesia imepanda na kufikia zaidi ya 1,400 Jumatano wiki hii kulingana na taakwimu za serikali.
Hata hivyo mambo mengi yanahitajika katika maeneo ya yaliyoathirika na zoezi la kutafuta miili ya watu waliofariki na manusura waliokwama chini ya vifusi vya nyumba linaendelea.
Mamlaka imetoa muda hadi Ijumaa, wiki moja baada ya kutokea tukio hilo, ili kuwapata watu ambao inawezekana kuwa wamenusurika.
Watu 1,600 walihamishwa kupitia bahari na meli ya kijeshi ya Indonesia ambayo iliweza kuegesha, ikiwa ilibeba misaada ya kibinadamu, katika mji wa pwani wa Palu.
Serikali nchini Indonesia imesitisha Ijumaa utafutwaji wa manusura wa tetemeko hilo na tsumani.
Misaada inaingia katika maeneo yaliyoathirika kupitia uwanja wa ndege wa Palu licha ya kuwa nao uliharibika kwa kiasi.
Baadhi ya wahanga wa tukio hilo sasa wanaweza kupata maji safi na chakula.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |