Bunge la Uganda lapiga kura kudumisha kodi ya matumizi ya mitandao ya kijamii
Wabunge nchini Uganda wamepiga kura ya kudumisha muswada wa kodi ya matumizi ya mitandao ya kijamii na utumaji wa fedha kupitia mtandao wa internet, licha ya muswada huo kupingwa vikali na jamii.
Wabunge 164, wengi wao kutoka chama tawala nchini humo NRM walipiga kura kukubali kodi hiyo ya dola 0.05 za kimarekani kwa matumizi ya mitandao ya kijamii na asilimia 0.5 ya kodi kwa kutuma au kupokea pesa kwa mtandao wa internet.
Awali, serikali ya Uganda ilisema haitaondoa kodi hizo licha ya kupingwa na wananchi, lakini hata hivyo, imepunguza kiasi cha kodi ya kutoa pesa kutoka asilimia 1 mpaka 0.5.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |