Zambia yawasimamisha kazi zaidi ya watumishi wa umma 70 kwa upotevu wa pesa
Serikali ya Zambia imesema wiki hii kuwa zaidi ya watumishi wa umma 70 katika wizara ya elimu wamesimamishwa kazi baada ya kupotea kwa fedha za wafadhili zilizolengwa kwenye programu za hisabati na sayansi.
Akiongea na wanahabari msemaji wa rais Amos Chanda amesema miongoni mwa waliosimamishwa kazi ni pamoja na katibu wa kudumu Henry Tukombe ambaye rais Edgar Lungu ameelekeza kupewa likizo ili kupisha ukaguzi wa ndani wa mahesabu juu ya suala hilo.
Wiki iliyopita waziri wa fedha Margaret Mwanakatwe alisema wafadhili wamesita kufadhili takriban dola milioni 13.9 za Kimarekani katika sekta ya elimu na Uingereza imesitisha ufadhili wake kwa wizara hiyo kufuatia madai ya kupotea kwa fedha hizo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |