Sahle-Work Zewde achaguliwa rais Ethiopia
Wabunge nchini Ethiopia wiki hii wamemchagua Sahle-Work Zewde kuwa rais wa kwanza mwanamke Ethiopia.
Bi Sahle-Work ni mwanadiplomasia mwenye uzoefu ambaye sasa amekuwa kiongozi wa kipekee mkuu mwanamke barani Afrika.
Kuchaguliwa kwake katika wadhifa huo kunajiri wiki moja baada waziri mkuu Abiy Ahmed kuliteua baraza la mawaziri ambapo nyadhifa nusu katika baraza hilo zimewaangukia wanawake.
Katika hotuba yake ya kukubali wadhifa huo, rais Sahle-Work amezungumza kuhusu umuhimu wa kudumisha amani, vyombo vya habari nchini vinaeleza.
Amechaguliwa baada ya kujiuzulu ghafla kwa kiongozi aliyekuwepo Mulatu Teshome.
Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat amepongeza kuchaguliwa kwa Bibi Sahel-Work Zewde akisema ni siahara muhimu katika kuwatambua wanawake.
Akiapishwa mbele ya wajumbe wa mabaraza ya bunge la nchi hiyo, rais Zewde ameahidi kufanya juhudi kadiri awezavyo kwa ajili ya taifa na wananchi wake.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |