Ebola yauwa 159 DRC
Idadi ya watu waliopoteza maisha Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, inaendelea kuongezeka.
Hadi siku ya Jumanne idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia ugonjwa wa Ebola ilikuwa imefikia 159, kulingana na ripoti ya tarehe 23 Oktoba 2018 ya shirika la Afya duniani (WHO) .
Wiki mbili zilizopita, WHO ilionya kuwa, kuna hatari ya maambukizi hayo kuendelea kuenea iwapo visa vya maambukizi havutapungua.
Mapema wiki hii Umoja wa Ulaya ulisema unatoa Euro Milioni 7.2 kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Msaada wa Umoja wa Ulaya unajumuisha ujuzi wa kiufundi, huduma za angani za kibinadamu, ufadhili wa utafiti na usaidizi wa kibinadamu, ameeleza Christos Stylianides, Kamishna anayehusika na Misaada ya kibinadamu na kukabiliana na Mgogoro katiak umoja wa Ulaya.
Fedha hizo zitasaidia masharika ya afya yanayofanya kazi ya kupambana na maambukizi haya, kuwaajiri watu zaidi kuwasaidia wagonjwa lakini pia kutoa elimu.
Mkoa wa Kivu Kaskazini ndio uanaathiriwa hasa Wilaya ya Beni, na idadi ya watu walipoteza maisha inaendelea kuongezeka kila kukicha.
Hata hivyo, Shirika la Afya Duniani linasema maambukizi hayo hayajafikia kiwango cha kutisha na kuathiri maeneo mengine duniani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |