NATO yafanya mazoezi makubwa zaidi ya kijeshi tangu Vita Baridi
Jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi NATO imeanza mazoezi ya kijeshi ya wiki mbili nchini Norway na kwenye maeneo ya karibu, yakiwa ni mazoezi makubwa zaidi ya kijeshi kufanyika tangu Vita Baridi ilipomalizika.
Taarifa ilitolewa na NATO inasema wanajeshi wapatao elfu 50, ndege 250, manowari 65 na magari elfu kumi ya kijeshi kutoka nchi 29 wanachama wa NATO na nchi washirika wake wawili Sweden na Finland, zitashiriki kwenye mazoezi hayo.
NATO inasema mazoezi hayo yanalenga kutathmini uwezo wake wa kuisaidia nchi mwanachama kurejesha mamlaka baada ya kuvamiwa kijeshi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |