Spika wa bunge la Somalia aapa kuendelea na kura ya kutokuwa na imani na rais
Spika wa bunge la Somalia Mohamed Mursal ameapa kuendelea na uungaji mkono wa hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais wa nchi hiyo Abdullahi Mohamed Farmajo na kuwahakikishia wabunge kuwa hoja hiyo inafuata katiba ya muda, sheria na taratibu za bunge.
Tangu Jumapili usiku wabunge 92 kati ya 275 wanaomba kupigwa kura ya kutokuwa na imani naye.
Katika barua kwa wabunge, Mursal amesema hoja ya kumpigia kura rais Farmaji ni halali licha ya wabunge 14 walioripotiwa kuwa wameunga mkono hoja hiyo na baadaye kukanusha madai hayo, na kuwa haikukidhi matakwa ya katiba ya nchi hiyo.
Hoja hiyo imesababisha mvutano wa kisiasa nchini humo iliyo katika pembe ya Afrika huku baadhi ya wabunge wameanza juhudi za upatanishi kwa ofisi za bunge na rais.
Mapema mwezi Novemba, Rais Farmajo alikutana na wenzake kutoka Eritrea Issaias na Waziri Mkuu wa Ethiopia Ahmed Abiy katika mkutano Kaskazini mwa Ethiopia wenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa kikanda kiuchumi kati ya nchi zao baada ya miaka kadhaa ya uhasama.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |