China yapeleka askari 100 wa kulinda amani nchini Sudan
Askari 100 wa kulinda amani wa China wameondoka leo hapa Beijing kuelekea Darfur, nchini Sudan kwa ajili ya majukumu ya ulinzi wa amani yatakayodumu kwa mwaka mmoja.
Askari hao ni kikundi cha kwanza cha timu ya askari 225, na ni kikosi cha 15 cha China kwenda mkoani Darfur, kikundi cha pili kinatarajiwa kuondoka China Disemba 18.
Kikosi hicho kitakuwa na jukumu la kusimamia mahitaji na miradi ya ukandarasi, kukarabati majengo, na kukarabati pamoja na kujenga nyumba, barabara, na viwanja vya ndege.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |