Rais Emerson Mnangagwa wa Zimbabwe asema hakuna uwezekano wa kuunda serikali ya umoja
Rais Emerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema chama tawala cha ZANU-PF hakina mpango wa kuwaalika wapinzani kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, kutokana na kuwa kilipata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi uliofanyika Julai 30.
Bw. Mnangagwa alimshinda kidogo mpinzani wake Bw Nelson Chamisa wa chama cha MDC, lakini chama chake kilipata wingi wa theluthi mbili ndani ya bunge, na kupata vingi vya serikali za mitaa, isipokuwa katika maeneo ya mijini ambako chama cha MDC kinadhibiti.
Hata hivyo vyama vya upinzani vinataka Rais Mnangagwa ajadiliane na wapinzani kuhusu namna ya kutatua matatizo ya nchi, kwa kuwa chama tawala kimeshindwa kufanya hivyo. Rais Mnangagwa amesema chama cha ZANU-PF kilishinda uchaguzi na kina dhamana ya kutawala peke yake katika miaka mitano ijayo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |