Afrika Kusini yajiunga na mpango wa soko huria la Afrika
Kitengo cha biashara na viwanda (DTI) kimeeleza kuwa Afrika kusini imethibitisha kukubaliana na mpango wa kuanzisha eneo la soko huria la Afrika.
Afrika ya kusini imefikia maamuzi hayo katika mkutano wa mawaziri wa biashara wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika jijini Cairo Misri desemba 12 na 13 na kuwa ni rasmi sasa Afrika Kusini imekuwa imejiunga kwa mujibu wa sheria.
waziri wa biashara na viwanda wa Afrika Kusini Rob Davies ameeleza kuwa, kutokana na juhudi zilizofanywa Afrika Kusini inaelekea kupanua ushirikiano zaidi ya jumuiya zilizopo za kikanda na kufanya kazi kuelekea kuanzishwa kwa maeneo makubwa ya soko huria barani Afrika.
Mpango wa eneo la soko huria la Afrika ulianzishwa mwezi Juni mwaka 2015 mjini Sharm El Sheikh Misri na inakusudia kuunganisha bara la Afrika na kuunda soko kubwa la watu milioni 626 lenye jumla ya bidhaa za ndani za dola za Marekani trilioni 1.2
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |