Uchaguzi wa DRC waahirishwa katika baadhi ya maeneo
Tume ya uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (CENI) imesema, kutokana na athari ya kuenea kwa ugonjwa wa Ebola na mapambano ya umwagaji damu kati ya makabila, upigaji kura katika sehemu za kaskazini mashariki na magharibi mwa nchi hiyo utaahirishwa hadi mwezi wa Machi mwakani.
Taarifa iliyotolewa na tume hiyo imesema, matokeo ya upigaji kura wa urais yatatangazwa tarehe 15, mwezi Januari mwakani na rais mpya ataapishwa tarehe 18, mwezi huo.
Tume hiyo pia imesema, kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya nchi hiyo, matokeo ya uchaguzi hayataathiriwa na hali ya kuwepo kwa maeneo yanayoshindwa kupiga kura kutokana na matatizo mbalimbali.
Jeshi na polisi wamezima maandamano ya wakazi wa Beni waliokuwa wameingia mitaani kupinga hatua ya Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) ya kuahirisha uchaguzi katika maeneo ya Beni, Butembo (mashariki mwa DRC) na Yumbi (magharibi mwa nchi).
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |