Uturuki iko tayari kuendelea kupambana na IS nchini Syria baada ya askari wa Marekani kuondoka
Uturuki imetuma askari wengi katika maeneo ya mpaka na Syria ili kujiandaa kuendelea na vita dhidi ya kundi la IS baada ya askari wa Marekani kuondoka Syria.
Rais Donald Trump wa Marekani wiki iliyopita alishangaza serikali yake na wenzi wa kimataifa baada ya kutangaza kuwa askari elfu 2 wa vikosi maalumu wa Marekani nchini Syria wataondoka na mashambulizi ya anga dhidi ya IS yatasimamishwa katika siku 60 hadi 100 zijazo.
Uamuzi huo umesababisha kujiuluzu kwa waziri wa ulinzi Bw. Jim Mattis na mjumbe wa muungano wa kimataifa wa kupambana na IS Bw. Brett McGurk.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |