Ujumbe wa serikali ya Yemen wafika Hodeidah kujiunga na ujumbe unaoongozwa na UN kusimamia usimamishaji vita
Ujumbe wa serikali ya Yemen umefika wiki hii katika mji wa Hodeidah, kujiunga na kamati ya pamoja inayoongozwa na Umoja wa mataifa kusimamia utekelezaji wa usimamishaji wa vita. Ujumbe wa serikali wenye watu watatu, uliingia mjini Hodeidah kwa maderaya ya Umoja wa mataifa.
Jenerali mstaafu wa Uholanzi Patrick Cammaert anayeongoza tume ya umoja wa mataifa, anajiandaa kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na mahasimu wa pande mbili, yaani serikali ya Yemen inayoungwa mkono na Saudi Arabia, na kundi la Houthi linaloungwa mkono na Iran.
Kwa mujibu wa makubaliano ya kusimamisha vita, kuondoa wapiganaji kutoka bandari za Hodeidah, Salif na Ras Issa pamoja na sehemu nyingine muhimu za mji huo, kutakuwa ni hatua ya kwanza na kunatakiwa kukamilika ndani ya wiki mbili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |