Sherehe ya kutawazwa kwa rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imefanyika Alhamisi, Januari 24 mchana kwenye makao makuu ya ofisi ya rais.
Felix Tshisekedi anakuwa rais wa tano wa nchi hiyo, lakini wa kwanza katika historia ya nchi hiyo kidemokrasia.
Katika hotuba yake ya kuapishwa, ambayo ilidumu karibu saa moja na ambapo alipata hitilafu ya kiafya, amekaribisha siku hiyo ya kihistoria.
Amemrithi Joseph Kabila ambaye ameondoka madarakani baada ya kuwa madarakani miaka 17.
Imekuwa mara ya kwanza nchi hiyo kushuhudia mabadiliko ya madaraka kwa amani, kutoka rais mmoja kwenda mwingine, tangu ilipopata uhuru mwaka 1960. Licha ya kuingia madarakani, Tshisekedi mwenye umri wa miaka 55, anaanza kazi kubwa ya kuongoza nchi hiyo yenye utajiri mkubwa rasimali, lililogawanyika kisiasa.
Katika hotuba yake, rais Tshisekedi ameahidi kuliunganisha taifa hilo na kuhakikisha kuwa amani inarejea lakini pia uchumi unaimarika.
Wakati wa hotuba yake, alilazimika kuikatisha baada ya kuugua ghafla jukwani lakini, baada ya muda mfupi akarejea tena na kuendelea na hotuba yake.
Martin Fayulu, aliyewania urais kupitia muungano wa Lamuka, anaamini kuwa alishinda Uchaguzi huo na hatambui ushindi wa Tshisekedi kwa sababu aliibiwa kura.
Viongozi wa Kanisa Katoliki, walisusia sherehe hizo , kwa kile walichosema kuwa hawaamini kuwa Tshisekedi alishinda Uchaguzi huo.
Hata hivyo sherehe hiyo imehudhuriwa na rais mmoja pekee, uhuru Kenyatta wa Kenya, kati ya marais 17 waliotajwa na wizara ya mambo ya nje ya DRC.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |