• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 20-January 25)

    (GMT+08:00) 2019-01-25 19:27:22

    Mazungumzo kati ya Korea Kaskazini na Marekani yamalizika nchini Sweden

    Waziri wa mambo ya nje wa Sweden Bw. Margot Wallstrom amesema mazungumzo kati ya wawakilishi wa Korea Kaskazini na Marekani yamefanyika jumatatu wiki hii, kwenye mazingira mazuri.

    Kituo cha radio cha Sweden kimemnukuu Bw. Wallstrom akisema, mazungumzo hayo yanalenga kuhimiza kuunda mawasiliano ya karibu zaidi kati ya pande hizo mbili na yanahusiana na kupunguza silaha za nyuklia, na maendeleo ya uchumi na usalama wa kikanda.

    Habari nyingine zinasema, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Michael Pompeo amesema, mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini yaliyofanyika nchini Sweden yamepata maendeleo, lakini pia alisisitiza kuwa hivi sasa pande hizo mbili zinakabiliana na masuala mengi.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako