• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February 9-February 15)

    (GMT+08:00) 2019-02-15 21:02:03
    Tume ya Taifa ya Uchaguzi DRC yakagua hali ilivyo Yumbi

    Tume ya Taifa ya Uchaguzi ncini DRC (CENI) imeanza maandalizi ya uchaguzi wa wabunge na wakuu wa mikoa katika maeneo ya Beni na Butembo katika mkoa wa Kivu Kaskazini na katika eneo la Yumbi katika mkoa wa Mai Ndombe.

    Wakaazi wa Beni na Butembo hawakupiga kura mwezi Desemba 2018 kwa sababu ya mlipuko wa Ebola na ongezeko la makundi ya watu wenye silaha, kulingana na maelezo ya viongozi wa DRC. Katika eneo la Yumbi, machafuko kikabila yaliua watu zaidi ya 800. Jengo na vifaa vya Tume ya Uchaguzi (CENI) vilichomwa moto. Tume ya Uchaguzi inajiandaa kuendesha mchakato huo machi 31, 2019.

    Ujumbe wa Tume ya Uchaguzi (CENI) uliwasili Yumbi siku ya Alhamisi. Lengo lake ni kutathmini changamoto za usalama na vifaa kabla ya uchaguzi wa wabunge na magavana wa mikoa Machi 31, miezi minne baada ya machafuko ya kikabila.

    Kazi ya kwanza: kuhakikisha kuwa hali ya usalama iko shwari katika eneo hilo ambalo kwa sasa linaoongozwa na afisa wa cheo cha kanali kutoka jeshi la DRC (FARDC) ambaye aliteuliwa mkuu wa wilaya baada ya machafuko.

    Hapa, watu wachache waliobaki katika mji huko baada ya machafuko wanahofu ya kutokea kwa shambulio jingine licha ya idadi kubwa ya jeshi na maafisa aw polisi pamoja na walinda amana wa Umoja wa Mataifa kutumwa katika eneo la Yumbi. Kazi kubwa nyingine ni kuwahamasisha wakaazi waliotoroka makazi yao kurejea haraka kabla ya uchaguzi.

    Kwa mujibu wa msemaji wa Monusco, hali hiyo inaweza kuchukuwa muda mrefu kutokana na kiwango cha uharibifu katika eneo hilo, kupotea kwa mali nyingi za watu na ukosefu wa huduma za serikali. Lakini pia uharibifu wa jengo na vifaa vya Tume ya Uchaguzi. Pia kuna kazi ya kuwatafuta wafanyakazi wengine wa CENI katika eneo hilo.

    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako