Venezuela yatafuta uungaji mkono wa kimataifa katika UM
Venezuela inajaribu kutafuta uungaji mkono katika Umoja wa Mataifa wakati msukosuko wa kisiasa unatokea nchini humo.
Akisoma taarifa kwa waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York mbele ya wawakilishi kutoka nchi nyingine 16, waziri wa mambo ya nje wa Venezuela Bw. Jorge Arreaza amesema kundi moja muhimu la nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa linafuatilia kwa karibu hitaji la kudumisha heshima kwa katiba ya Umoja wa Mataifa inayooongoza mwenendo wa jumuiya ya kimataifa, na limeamua kuchukua hatua za uratibu kulinda katiba hiyo na haki za nchi wanachama wote, ikiwemo haki za usawa na wananchi kujiamulia mambo yao, kuheshimu usawa wa mamlaka ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na kutoingilia masuala ya nchi nyingine.
Wakati huo huo Rais Nicolas Maduro wa Venezuela ameitaka nchi hiyo kutokuwa na hofu ya vita na kudumisha hali ya amani.
Akizungumza mjini Caracas, Rais Maduro pia ameutaka upande wa upinzani utafute njia ya amani kwa kutatua mgogoro wa siasa nchini humo.
Wakati huohuo, waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergei Lavrov alizumgunza na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo kwa njia ya simu, na kuionya Marekani isiingilie kati mambo ya ndani ya Venezeula. Pia alieleza kuwa misaada ya kibinadamu ambayo Marekani inapeleka nchini Venezeula inalenga kuvunja utulivu wa nchi hiyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |