Rais wa Kenya aamuru wauguzi warudi kazini
Rais Uhuru Kenyatta amewaamuru wauguzi wanaogoma nchini humo warudi kazini kabla ya Ijumaa, la sivyo watakabiliwa na hatua za kinidhamu.
Rais Uhuru ameitisha mkutano wa dharura na viongozi wa wizara ya afya na kamati ya magavana, na kuagiza polisi wa nchi hiyo kuchukua hatua kali dhidi ya vitendo vya kuzuia wauguzi kurudi kazini. Amesema wauguzi wanaoshindwa kurudi kazini kutokana na amri yake watafutwa kazi na serikali za mitaa na wizara ya afya.
Mgomo wa wauguzi umeingia wiki ya pili, na umeleta athari kwa utoaji wa huduma muhimu kwenye hospitali za kiserikali, ambapo watu wenye kipato cha chini wanasubiri kupata matibabu. Katibu mkuu wa Shirikisho la Wauguzi la Kenya Bw. Seth Panyako amesema, wanachama wake hawataacha madai yao kutokana na makubaliano waliyofikia na waajiri wao.
Hata hivyo, rais Uhuru ametangaza mgomo huo ni haramu, kwa kuwa umekiuka amri ya kusitishwa iliyotolewa na mahakama ya uhusiano wa ajira na leba.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |