• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February 9-February 15)

    (GMT+08:00) 2019-02-15 21:02:03

    Zaidi ya wafanyakazi 6,000 nchini Afrika Kusini huenda wakapoteza ajira kutokana na marekebisho ya Kampuni ya Sibanye-Stillwater

    Zaidi ya wafanyakazi 6,000 wa mgodi nchini Afrika Kusini huenda watapoteza ajira zao kutokana na marekebisho ya Kampuni ya Sibanye-Stillwater.

    Sibanye-Stillwater ni kampuni kubwa zaidi ya uzalishaji wa dhahabu nchini Afrika Kusini, na moja ya kampuni kumi kubwa za uzalishaji wa dhahabu duniani. Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo inasema, kutokana na hasara, majadiliano kuhusu marekebisho ya kampuni hiyo yatafanyika, na marekebisho hayo yanaweza kuwaathiri wafanyakazi karibu elfu 6000.

    Habari nyingine zinasema idadi ya vifo vya watu kutokana na mlipuko wa gesi chini ya mgodi wa makaa ya mawe wa Gloria mkoani Mpumalanga, Afrika Kusini imefikia 12. Mlipuko huo ulitokea tarehe 7 kwenye mgodi huo ulioachwa mwaka jana. Hadi sasa watu 10 wengine bado wako kilomita mbili chini ya mgodi huo.

    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako