Trump na Kim wakosa mwafaka
Mkutano kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un umemalizika bila kufikia makubaliano baada ya Marekani kukataa kutoa nafuu ya vikwazo kwa Korea Kaskazini, Rais wa Marekani ameeleza.
''Ilikuwa ni kuhusu vikwazo,'' Trump aliwaambia wanahabari.''Walitaka kuondolewa vikwazo na hatukuweza kufanya hivyo.''
Wawili hao walikua wanatarajiwa kutangaza maendeleo kuhusu mipango ya kukomesha matumizi ya silaha za Nuklia.
Trump amesema hakuna mipango yoyote iliyowekwa kwa ajili ya kufanyika kwa mkutano wa tatu.
Mipango ya awali ya Ikulu ya Marekani ilikua ni maandalizi ya sherehe za ''utiaji saini makubaliano'' pia chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya viongozi hao wawili, lakini matarajio yao yalizimwa kutokana na kuahirishwa kwa mkutano huo.
Kwa Mujibu wa Trump, Kim alitoa ahadi muhimu- kuondoa vinu vya Yongbyon , vinavyotumika kufanya utafiti na uzalishaji Korea Kaskazini.Lakini kwa upande wake Kim alitaka vikwazo vyote viondolewe, kitu ambacho Marekani haikujiandaa kufanya hivyo.
Eneo la Yongbyon nchini Korea Kaskazini ni maarufu kwa upatikanaji wa kemikali ya plutonium lakini nchi hiyo ina takriban vinu viwili vinavyozalisha Uranium.
Pia rais Trump amesema kuwa Kim aliahidi uteketeza vinu vya Yongbyon pekee na si vinu vyote vya nuklia vya Korea Kaskazini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |