• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February23-March 1)

    (GMT+08:00) 2019-03-01 16:23:01

    Chama kikuu cha upinzani cha Nigeria chakataa matokeo ya uchaguzi wa urais

    Chama kikuu cha upinzani cha Nigeria PDP kimekataa matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika wikiendi iliyopita mjini Abuja.

    Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Uche Secondus ametoa taarifa akisema matokeo ya uchaguzi yaliyokusanywa na yanayopitiwa na tume huru ya uchaguzi INEC hayaaminiki na yana makosa, na chama chake na wananchi hawatayakubali. Chama cha PDP kimesema matokeo yanayotangazwa na tume ya INEC yanakwenda kinyume na matokeo yaliyokusanywa nacho..

    Msemaji wa tume ya uchaguzi Bw. Rotimi Oyekanmi amesema mchakato wa uchaguzi umesimamiwa na waangalizi wa ndani na wa nje, na matokeo yake ni halali. Matokeo kutoka majimbo kumi yametolewa, na mengine yatatolewa baadaye. Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutangazwa kabla ya kesho.

    Wananchi wa Nigeria wanasubiri ahadi rais wao alizozitoa kama zitatekelezwa.

    Muhammadu Buhari mwenye umri wa miaka 76 alichaguliwa kwa muhula wa pili. Mwaka 2015, kuchaguliwa kwake kulifufua matumaini mengi, na kuonyesha ishara ya kupishana kwenye madaraka kwa njia ya kidemokrasia. kuchaguliwa kwake kwa muhula wa pili kunaonekana kama chanzo cha utulivu, hata kama matokeo ya sera yake yamekuwa yakikosolewa na wengi.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako