Marekani na kundi la Taliban nchini Afghanistan zaendelea kufanya mazungumzo kuhusu kuondoa majeshi
Msemaji wa kundi la Taliban nchini Afghanistan Zabiullah Mujahid amesema, duru ya tano ya mazungumzo kati ya Marekani na kundi la Taliban nchini Afghanistan imeendelea kufanyika huko Doha, nchini Qatar.
Bw. Mujahid ameandika kwenye mtandao wa kijamii kuwa, pande hizo mbili zimefanya majadiliano kuhusu kuondoa jeshi la Marekani nchini Afghanistan na kutoathiri vibaya nchi nyingine kwa kutumia ardhi ya Afghanistan. Lakini hakuweka wazi mambo muhimu yaliyojadiliwa na matokeo ya mazungumzo hayo.
Mwezi Januari serikali ya Marekani na wakilishi wa kundi la Taliban nchini Afghanistan walifanya mazungumzo ya duru ya nne huko Doha. Kwa mujibu wa habari zilizotolewa na kundi la Taliban, baada ya mazungumzo ya siku sita, pande hizo mbili zilisaini muswada wa makubaliano unaolenga kukomesha vita nchini Afghanistan.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |