Ndege mbili za India zadenguliwa na Pakistan
Pakistani imemwachilia rubani wa ndege ya kivita iliodenguliwa na jeshi la Pakistan kwenye eneo linalozozaniwa la Kashmir.
Serikali ya Pakistan imesema imemwachilia rubni huyo kama ishara ya kutaka suluhu la amani kwenye mzozo huo.
Awali wiki hii ndege mbili za kivita za India zilidenguliwa na Pakistan kwenye eneo hilo la mpakani.
India na Pakistan zote zilizo na silaha za nyuklia kila moja inadai eneo lote la Kashmir lakini kila mmoja anadhibiti sehemu ya eneo hilo.
Wamepigana vita mara tatu tangu wapate uhuru kutoka Uingereza mwaka 1947.
Mashambulizi ya ndege kwenye mpaka unaogawanisha India na Pakistan nduyo ya kwanza tangu mwaka 1971.
Yanafuatia shambulizi la wanamgambo huko Kashmir lililowaua wanajeshi 40 wa India yakiwa ndiyo mabaya zaidi wakati wa kipindi cha miongo mitatu ya kupinga uwepo wa India huko Kashmir.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |