Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe wiki hii amekutana na wafanyabiashara na wadau wengine, na kuwataka watoe misaada zaidi kwa ukarabati wa miundombinu kutokana na uharibifu uliosababishwa na kimbunga Idai kilichotokea Machi.
Kampuni kadhaa zimeahidi kuchangia ukarabati wa shule na miundombinu iliyoharibiwa.
Kabla ya mkutano huo, serikali ya Zimbabwe imesema dola za kimarekani milioni 612 zinahitajika kwa ajili ya chakula, malazi na ukarabati wa miundombinu.
Hadi sasa idadi ya watu waliofariki kutokana na kimbunga hicho imefikia 344, na huenda ikaongezeka zaidi baada ya miili mingine kupatikana.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |