Rwanda yaadhimisha miaka 25 tangu kutekelezwa mauaji ya kimbari mwaka 1994
Rwanda yaadhimisha miaka 25 tangu kutekelezwa mauaji ya kimbari.
Miaka 25 yatimia tangu kufanyika mauaji ya kimbari nchini Rwanda, kila ifikapo Aprili 7 Rwanda huadhimisha siku ya kuwakumbuka wote waliouawa tangu April 7 mwaka 1994.
Mauaji hayo ya kimbari yalianza mwaka 1994, mauaji ambayo yalidumu kwa muda usiopungua miazi mine.
Watu zaidi ya millioni moja jamii ya watutsi waliuawa wakiwemo wahutu wenye misimamo ya wastani na wangambo waliokuwa wakishirikiana na utawala wa rais Habyarimana ambae aliuawa katika shambulizi lililolenga ndege yake kutoka mkoani Arusha nchini Tanzania akiwa pamoja na rais wa Burundi Cyprien Ntaryamira.
Rais wa Rwanda Paul Kagame amewapokea viongozi kutoka katika mataifa tofauti mjini Kigali akiwemo Mussa Faki kwa ajili ya kuadhimisha miaka 25 tangu kufanyika kwa mauji ya kimbari.
Shughuli za wiki nzima zilianza kwa Bw Kagame akiwasha mwenge wa makumbusho ambapo watu 250,000 wanaripotiwa kuzikwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |