Ethiopia kusaidia wakimbizi wa ndani milioni 2 wanaokabiliwa na uhaba wa chakula
Serikali ya Ethiopia wiki hii imetangaza juhudi zake zinazoendelea za kuwawezesha wakimbizi wa ndani milioni 2 waishi maisha ya kawaida.
Katika majadiliano na wanachama wa jumuiya ya kimataifa ya wafadhili, wizara ya amani ya Ethiopia imeomba msaada wa kifedha wa dola za kimarekani milioni 700, ili kuwasaidia watu zaidi ya milioni 2 walioathiriwa na migogoro na majanga ya asili.
Wiki iliyopita, Jumuiya ya maendeleo ya kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki IGAD ilionya kuwa Afrika Mashariki inakabiliwa na msukosuko mkubwa wa chakula, ambapo watu milioni 10.7 wanakabiliwa na ukosefu wa chakula. Vilevile ilizitaka nchi husika zichukue hatua za haraka ili kukabiliana na hatari ya ukosefu wa chakula kwenye sehemu za Ethiopia, Kenya, Somalia na Uganda kutokana na upungufu wa mvua.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |