Tanzania yajiandaa kwa uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika baadaye mwaka huu
Serikali ya Tanzania imesema, inapanga kutumia shilingi bilioni 82.9 za Tanzania katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Naibu waziri wa ofisi ya rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Mwita Waitara ameliambia bunge mjini Dodoma kuwa, maandalizi ya uchaguzi huo, ikiwemo kununua vifaa vya uchaguzi yanaendelea.
Bw. Waitara amesema hayo wakati akijibu swali la mbunge wa Mtambile Bw. Masoud Abdallah Salim aliyetaka kujua maandalizi yanayofanywa na serikali kwa ajili ya uchaguzi huo.
Bw. Waitara amesema, serikali imeandaa kanuni zitakazotumiwa kwenye uchaguzi na mafunzo kwa maofisa watakaosimamia uchaguzi huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |