Kenya Uganda na Tanzania zasoma bajeti ya 2019/20
Mataifa ya jumuiya ya Afrika mashariki Uganda, Kenya na Tanzania yamewasilisha bajaeti zao za mwaka 2019/20.
Nchini Kenya Waziri wa Fedha Henry Rotich aliwasilisha makadirio ya bajeti ya dola bilioni 31.5 kwa mwaka wa 2019 hadi 2020 ambayo inatajwa kubwa zaidi.
Waziri Rotich amesema kuwa bajeti hiyo imezingatia ndoto na azimio la Rais Uhuru Kenyatta kuwekeza katika sekta nne muhimu ili kuliendeleza taifa.
Sekta hizo ni pamoja na zile za Afya, Kilimo, Makaazi na Uzalishaji wa viwanda na sekta hizo zimepewa sehemu kubwa ya mgao wa bajeti.
Nchini Tanzania waziri wa fedha Dokta Philip Mpango huku ikiwa na mapendekezo ya kufutwa kwa tozo tano pamoja na marekebisho ya baadhi ya sheria.
Katika Bajeti hiyo ya shilingi za kitanzania trilioni 33 serikali ya Tanzania imetenga shilingi trilioni 12.2 kwa ajili ya kugharamia mpango wa Maendeleo wa Taifa mwaka 2019/2020.
Kati ya fedha hizo shilingi trilioni 9.7 ni fedha za ndani na shilingi trilioni 2.5 ni fedha za nje.Fedha hizo za maendeleo ni sawa na asilimia 37 ya bajeti yote ya mwaka 2019/2020.
Bajeti ya Uganda ilipitishwa mwezi wa Mei lakini kwa ujumla waziri wa fedha wa Uganda Matius Kassaja ameangazia zaidi masuala ya ujenzi wa viwanda na alisema kuwa Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2019 na 2020 inalenga hatua zinazokusudia kuongeza utajiri na na ustawi wa waganda wote.
Pia ameongezea kuwa biashara baina ya Uganda na nchi za Afrika Mashariki imeongezeka hadi 59% ya bidhaa zote zilizosafirishwa mwaka 2018.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |