• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 8-Juni 14)

    (GMT+08:00) 2019-06-14 19:52:18

    China yalalamikia kauli yenye makosa ya Umoja wa Ulaya kuhusu Hongkong kufanya marekebisho ya sheria

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inapinga kithabiti kauli ya makosa ya Umoja wa Ulaya kuhusu Hongkong kufanya marekebisho ya sheria ya kukamata wahalifu wanaotoroka, na sheria ya kushirikiana kisheria katika mambo ya kesi za jinai, kuwa huenda kutaathiri watu wa Hongkong.

    Bw. Geng Shuang amesema, mambo ya Hongkong ni mambo ya ndani ya China, na nchi yoyote na mashirika na mtu yeyote hana haki ya kuingilia. Amesema China inautaka Umoja wa Ulaya kujizuia maneno yake, kuacha kuingilia kati mambo ya Hongkong na mambo ya ndani ya China.

    Awali Bw. Geng Shuang alisema China inaitaka Marekani ifikirie serikali ya eneo maalumu ya Hong Kong kusahihisha sheria kwa haki, kuchunga maneno yake, na kusimamisha kuingilia kati mambo ya Hong Kong na mambo ya ndani ya China.

    Bw. Geng Shuang amesema, China imeeleza msimamo wake mara kwa mara kuhusu eneo maalumu la Hong Kong kusahihisha sheria. Serikali ya Hong Kong imesikiliza maoni ya pande mbalimbali za jamii, na kutoa majibu kwa mapendekezo husika. Amesema serikali kuu ya China itaendelea kuunga mkono serikali ya eneo maalumu ya Hong Kong kuendelea na kazi hiyo.

    Habari zinasema, wizara ya mambo ya nje ya Marekani hivi karibuni imeeleza wasiwasi wake kuhusu Hong Kong kusahihisha sheria ya kukamata wahalifu wanaotoroka, na inaona hatua hiyo itaathiri hadhi maalumu ya Hong Kong katika mambo ya kimataifa.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako