Sudan Kusini wiki hii imesaini makubaliano na Kituo cha Kikanda cha Silaha Ndogo (RCESA) ili kuimarisha juhudi za kuridhia Mkataba wa Biashara ya Silaha (ATT) na kupunguza migogoro na uhalifu wa kimabavu.
Mwenyekiti wa Mamlaka ya usalama wa jamii na udhibiti wa silaha ndogo Andrew Kuol Nyuon amesema, mamlaka hiyo inafanya operesheni nchini kote ili kuwahimiza wadau wakuu kutambua haja ya kuunga mkono mkataba wa kupiga marufuku biashara haramu ya silaha ndogo.
Nyuon amesema asilimia 70 ya vifo nchini Sudan Kusini vinatokana na biashara hiyo haramu, pia amesisitiza ofisi yake inafanya juhudi ili kudhibiti na kupunguza silaha ndogo na silaha nyepesi nchini humo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |