Zaidi ya watu 500 wakamatwa Misri
Watu zaidi ya 500 wamekamatwa katika maeneo mbalimbali nchini Misri kwa kipindi cha siku kadhaa zilizopita, wakati wa maandamano dhidi ya rais wa nchi hiyo Abdel Fattah al-Sisi.
Watetezi wa haki za binandamu wametoa takwimu hizo kutokana na maandamano yaliyofanyoka siku ya Ijumaa na Jumamosi iliyopita jijini Cairo na maeneo mengine ya nchi hiyo.
Miongoni mwa watu waliokamatwa ni mwanaharakati maarufu Mahienour el-Massry aliwahi kushinda tuzo ya Kimataifa.
Maafisa wa usalama wanamshtumu el Massry kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi lakini pia kuhusika na uchapishaji wa habari za uongo.
Waandamanaji nchini Misri wakati wa maandamano hayo, walikuwa wanalalamikia kuendelea kuteswa kwa wapinzani wa rais el Sisi, na kuzuiwa kushiriki katika maandamano dhidi ya utawala wake.
Maandamano nchini Misri, yamepigwa marufuku nchini Misri tangu mwaka 2013 wakati rais wa zamani Mohammed Morsi alipoondolewa madarakani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |